Waafrika kutengeneza drone Urusi

URUSI : TAKRIBAN wanawake 200 wenye miaka 18 hadi 22 kutoka barani Afrika, wanasajiliwa kwenda kufanya kazi Urusi.

Wanawake hao wanafanya kazi  katika kiwanda kinachohusika kuunda maelfu ya droni za Iran zinazotumika kuishambulia Ukraine.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti maalumu iliyotolewa na shirika la habari la Associated Press baada ya kukamilisha uchunguzi wake.

Advertisement

Katika mahojiano ya shirika la habari la AP baadhi ya wanawake wamesema walilaghaiwa kwamba wanakwenda Urusi katika programu ya kufanya kazi na kusoma na badala yake wameeleza kwamba wanafanya kazi kwa muda mrefu wakiwa chini ya uangalizi muda wote.

SOMA : Urusi yajipanga kudungua drone za Ukraine

Ripoti hiyo imebainisha kuwa, Urusi inayokabiliwa na uhaba wa nguvukazi katika kipindi hiki cha vita, kupitia Abaluga, imewaajiri wanawake kutoka Uganda, Rwanda, Kenya, Sudan Kusini, Sierra Leone na Nigeria, pamoja na Sri Lanka iliyo Kusini mwa bara la Asia.