Waagizwa kukamilisha miradi Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya mkoani humo kukamilisha miradi yote kwa wakati kabla ya kukamilika mwaka wa fedha wa 2022/2023 ambao utafikia tamati ifikapo Juni 30, 2023.

Senyamule ametoa maagizo katika kikao kazi na viongozi wa Halmshauri za Wilaya na Mji za Mkoa wa Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi Mei 25, 2023.

“Tumebakiwa na takribani mwezi mmoja wa kukamilisha miradi yote, kwa muda uliowekwa tunatakiwa kufanya haraka na kwa weledi kabla ya Juni 30, kwakuwa Mhe.

Rais Samia Suluhu Hassan anatafuta fedha kwa kasi kwahiyo na sisi aliotuteua kumsaidia tunatakiwa tufanye kazi kwa nguvu ili kumuunga mkono,” alisema Senyamule

Aliongeza; “Lazima tufanye ubunifu ili majengo ya miradi tuliyopatiwa fedha yakamilike kwa wakati na niwasisitize muwalipe mafundi fedha zao kwa wakati kwasababu ukishamlipa fundi atafanya kazi kwa weledi, vilevile tununue vifaa kwa wakati ili kuondoa ucheleweshaji wa namna yoyote ili iwe ikiwa ni pamoja na kuwakwamisha kuendelea na kazi zao kwa mujibu wa mpango kazi uliopo.” Amesema Senyamule

RC Senyamule aliwaasa viongozi hao kufanya uchambuzi wa vyanzo vyote ambavyo havikukusanya mapato na kuvitafutia namna nzuri ya kukusanya mapato huku akibainisha kuwa mkoa huo umekusanya mapato kwa asilimia 76 na asilimia 24 pekee zikisali.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button