Waandikishaji watakiwa kuwa waadilifu

MSIMAMIZI wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Murtallah Mbillu amewataka waandikishaji kuwa waadilifu na wasimuonee mwanachi mwenye sifa ya kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura.

Mbillu ametoa agizo hilo wakati wa kufungua mafunzo katika semina ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa waandikishaji na qasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na kuwataka kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria kanuni, pamoja na miongozo.

Amesema waandikishaji wote wanapaswa kuwa waadilifu bila kumuonea mwananchi yoyote mwenye sifa za kuandikishwa.

Advertisement

“Katekelezeni majukumu yenu kama miongozo inavyowataka, sheria, kanuni na kwa kuzingatia kiapo mlichokula leo, pia kaonyesheni uaminifu mkubwa kama mlivyoaminiwa na kuchaguliwa kuwa waandikishaji,”

Ikumbukwe zoezi la uandikishaji wapiga kura litaanza Oktoba 11 hadi 20 mwaka huu na uchaguzi wa kuchagua viongozi wa serikali za mitaa utafanyika Novemba 27 Novemba, 2024 kwenye Tarafa zote tatu ambazo ni Loliondo, Sale na Ngorongoro huku kauli mbiu ikiwa ni “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi”