Waandishi malkia wa nguvu Nyanda za Kusini
KILELE cha tuzo za Malkia wa Nguvu 2024 Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kimekamilishwa kwa malkia sita wa nguvu kukabidhiwa tuzo zao kwenye vipengele mbalimbali usiku wa Septemba 27 zilziofanyika ukumbi wa Eden Highland, Mbeya.
Tuzo hizo zilihudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa.
Vipengele hivyo ni pamoja na Kilimo Biashara tuzo aliyoshinda Mama Faustina Mahenge Mkulima aliyeanza na hekari 2 na kwa sasa ana maelfu ya hekari kwa ukubwa wa mashamba yake ana uwezo wa kulisha mkoa mzima wa Mbeya.
SOMA: Aibuka kinara malkia wa nguvu sekta binafsi
Biashara ya Chakula ameshinda Doris Luvanda aliyeanza biashara kama mama muuza chai na makande katikati ya stand ya Uyole akiwa na umri mdogo alipoteza wazazi wake wote wawili kwa sasa ni Milionea na ametoa ajira kwa mamia ya Watanzania.
Mwanamke mwenye ushawishi ameshinda Juliana Kibassa, mwanzilishi wa Taassi ya Sauti ya Mwanamke amekua akiendesha makongamano makubwa ya kumkomboa mwanamke kiuchumi na kijamii Upande wa Mjasiriamali bora ameshinda Albina Mughabe ambaye akiwa na miaka 14 familia yake ilimpatia Mume Tajiri ili aolewe yeye aligoma kuolewa ndipo familia ikamkana na kumtenga baadaye kituo cha Wamisionari cha Mt. Consolata kilimchukua kumlea na kumsomesha kwa sasa ni Mfanyabiashara mkubwa Mbeya mmiliki wa kampuni kubwa, shule, kituo cha afya na kiwanda cha kuzalisha tofali.
SOMA: Mama Maria Nyerere atunukiwa ‘Malkia wa Nguvu’ …
Mitindo na Urembo ameshinda Nasra Haonga ambaye alipata ujauzito akiwa kidato cha pili akafukuzwa nyumbani kwao baadae akaanza kupika pombe za Kienyeji bahati mbaya akapata matatizo yaliyompelekea kupelekwa jela miaka mitatu alipotoka alipambana kuanza upya kwa sasa ni Mfanyabiashara mkubwa wa maduka ya Nguo ya Nasra House of Fashion Mbeya.
Tuzo ya Ustawi wa Jamii ameshinda Noelah Shawa kwa zaidi ya miaka 30 amekua akiwasaidia watoto wenye changamoto ya ulemavu ambapo historia yake ilianza alipookota watoto wawili akiwa kidato cha pili aliwachukua na kuwapeleka nyumbani kwao na kuanza kuwalea kazi ambayo aliipenda kuifanya kwa sasa ana taasisi yake iitwayo Child Support Tanzania inayopokea watoto wenye changamoto mbalimbali za ulemavu.