Waandishi wa habari wafundwa haki, usawa uchaguzi mkuu

MTWARA: WAANDISHI wa Habari mkoani Mtwara wamepewa mafunzo kuhusu kuripoti kwa kuzingatia haki na usawa kwenye mchakato mzima wa uchaguzi mkuu naotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Haya yamejiri wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari hao kuhusu mbinu za kuripoti masuala hayo ya uchaguzi yaliyoandaliwa kwa pamoja baina ya Kampuni ya Media Brains ya Dar es salaam na taasisi ya Konrad Adenauer Stiftung ofisi ya Tanzania yaliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Aidha, miongoni mwa mada zilizotolewa kwenye mafunzo hayo ikiwemo sheria mpya ya uchaguzi wa Rais, wabunge pamoja na madiwani ya mwaka 2024 na sheria mpya ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwani lengo ni kuwajengea uelewa wa pamoja namna ambavyo wanaweza kuripoti habari hizo kwa weledi.
Mkurugenzi Mwenza wa Media Brains, Absalom Kibanda amewasisitiza wanahabari hao umuhimu wa kusoma kwa umakini sheria hizo ili wapate uelewa mzuri na kisha kuwaelimisha wananchi.
‘’Sheria hizi zimeanza kutumika kwenye mchakato wa awali wa uchaguzi hivyo ni muhimu wanahabari wakazifahamu ili kujilinda kisheria na kutekeleza majukumu yao kwa weledi,”amesema Kibanda.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Media Brains, Jesse Kwayu amewataka waandishi hao kuzingatia misingi na weledi ya waandishi wa habari kwenye uchaguzi huo ikiwemo kuangalia maslahi mapana ya nchi na kulinda amani.
Mkurugenzi Mwenza wa Media Brains, Neville Meena, amesema uelewa wa sheria hizo utasaidia wanahabari kuepukana hasa wakati makosa wanapowahoji wagombea na wadau mbalimbali huku akisisitiza umuhimu wa kuhakiki habari kabla ya kuchapishwa ili kuleta weledi wa kazi hizo.
Mafunzo hayo tayari yameshatolewa kwa waandishi wa habari katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mbeya, Kigoma, Mwanza, Kilimanjaro, Morogoro, Pwani , Lindi, Mtwara na mingine.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com