Waasi M23 wateka Goma, mpaka umefungwa

GOMA : MPAKA kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) na Rwanda umefungwa kufuatia mashambulizi ya waasi wa M23, ambao wamevamia jiji la Goma.
Kwa mujibu wa taarifa zilizozagaa, mpaka sasa hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia au kutoka kwenye mpaka huo kati ya nchi hizo mbili. SOMA:Tahadhari ya usalama yatangazwa Congo
Wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa na familia zao ndio pekee walioruhusiwa kuvuka, na walikuwa wakihamishwa kupitia Rwanda.
Shirika la utangazaji la serikali ya Rwanda limeripoti kuwa baadhi ya mabasi yalikuwa yanawasubiri wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na familia zao ili kuwahamisha kutoka Goma.


