Wabunge wasisitiza matumizi ya gesi asilia viwandani

DAR ES SALAAM: KAMATI ya kudumu ya bunge ya nishati na madini imeishauri wawekezaji wa viwanda kutumia gesi asilia ili ipunguze gharama za bei ya nishati na iwe tija kwao.

Hayo ameyasema Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kudumu ya nishati na madini, David Mathayo Machi 16 jijini Dar es salaam wakati kamati hiyo ilipotembelea viwanda vinavyotumia gesi kiwanda cha MMI Steal kinachozalisha mabati na Tanpack kinachozalisha tishu.

Aidha Mwenyekiti huyo ameongezea kwa kusema kuwa serikali iendelee kusambaza gesi kwa wingi viwandani kutokana na gesi inazalishwa hapa nchini.

Amesema Watanzania wanaotumia gesi hiyo ni wachache hivyo waendelee kuitumia kwa wingi na hivyo amewashauri shirika la Petroli Tanzania TPDC waendelee kusambaza gesi hiyo kwa wingi.

Nae Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, James Mataragio amesema ziara hiyo ya siku mbili imekuwa na manufaa makubwa na serikali imejipanga kuhakikisha gesi inawafikia wananchi  kwa uunganishaji wa gesi nyumbani na kwenye viwanda vyote.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Petroli Tanzania TPDC, Mussa Makame amesema utaratibu wa usambazaji wa gesi kwa mujibu wa sheria ya gesi ya mwaka 2015 inawashirikisha watu binafsi kwenye uwekezaji wa gesi hiyo.

Ziara hiyo hiyo ya kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini ilianza jana kwa kutembelea vituo viwili vinavyojaza gesi na kutamatika leo kwa kutembelea viwanda viwili vinavyotumia gesi.

 

Habari Zifananazo

Back to top button