Wabunge wagoma kupitisha hali ya tahadhari

KOREA KUSINI : RAIS wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol, ametangaza kuondoa sheria ya kijeshi nchini humo, hatua ambayo ilichukuliwa saa chache baada ya kuitangaza.
Hatua hii inakuja kufuatia shinikizo kutoka kwa wabunge 190 wa Bunge la Kitaifa la Korea Kusini, ambao walikubaliana kwa kauli moja kupinga sheria hiyo.
Rais Yoon alikubali ombi la Bunge na kusema atatekeleza kuondoa sheria hiyo kupitia mkutano wa baraza la mawaziri. SOMA: Rais Yoon Suk atangaza hali ya hatari
Katika upande mwingine, chama kikuu cha upinzani nchini humo Democratic Party, kimemtaka Rais Yoon kujiuzulu au apigiwe kura ya kura ya kutokuwa na imani naye kutokana na hatua yake ya kutangaza sheria ya kijeshi.
Wanachama wa chama hicho wameeleza kwamba Rais Yoon Suk ameshindwa kuongoza nchi kwa njia inayozingatia demokrasia, na wanasema kwamba hatua yake inapingana na misingi ya haki za kiraia.
Katika hotuba yake, Rais Yoon alisisitiza kwamba alitangaza hali ya tahadhari nchini Korea Kusini kutokana na kile alichokiita jaribio la upinzani la kuhujumu serikali yake, jambo ambalo linazidi kuongeza mivutano ya kisiasa katika nchi hiyo.



