KOREA KUSINI : RAIS wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol, ametangaza hali ya hatari ili kuilinda nchi dhidi ya vikundi vya kikomunisti vya Korea Kaskazini na kuondoa wapinzani wa serikali wanaokwenda kinyume na katiba ya nchi.
Hatahivyo ,vyombo vya habari nchini humo ikiwemo Yonhap, vimeripoti kuwa jeshi limetangaza kusimamisha shughuli za bunge na kuzuia wajumbe kuingia kwenye jengo la bunge, huku maafisa wa usalama wakiwa wanashika doria.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Democratic Party, Lee Jae-myung, amekosoa uamuzi huo akisema ni kinyume cha katiba. SOMA: Korea Kusini yapiga marufuku ulaji nyama ya mbwa
Viongozi wa chama tawala, wakiwemo Han Dong-hoon, wameapa kupinga hatua hiyo.
Yoon, ambaye alikosa nguvu bungeni baada ya kushindwa uchaguzi, anashutumiwa kwa kushindwa kupitisha sheria na kukumbwa na kashfa, ikiwemo ya mkewe inayohusiana na ufisadi.
Kambi ya upinzani nchini humo imeamua kuzuia bajeti na wanajiandaa kumchunguza mke wa rais.