Wachimbaji madini walazimika kula nyama ya binadamu, mende

AFRIKA YA KUSINI : WACHIMBAJI madini watatu kutoka mgodi wa Buffelsfontein huko Stilfontein, Afrika Kusini, wamesema kuwa hali ya uchimbaji chini ya ardhi ilikuwa mbaya kutokana na ukosefu wa huduma muhimu za kibinadamu na kulazimika  kula nyama ya binadamu na mende wakati wote..

Tangu Agosti mwaka jana, polisi wamezuia chakula na bidhaa nyingine kufikishwa kwa wachimbaji madini wanaodaiwa kuingia kwenye migodi ya Buffelsfontein iliyotelekezwa.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu na wanaharakati wa ndani wamesema kuwa vitendo vya polisi ni kinyume na haki za binadamu na vinapaswa kuepukika.

Advertisement

SOMA: Uwekezaji mkubwa sekta ya madini mapato yaongezeka