Wadau waendelea kutoa elimu ukatili wa kijinsia
WADAU mbalimbali wanaofanya shughuli za kupinga ukatili wa kijinsia mkoani Mtwara wamesema, wanaendelea kutoa elimu kwa jamii na kupunguza kasi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa na baadhi ya jamii hiyo mkoani humo.
Hayo yamejiri wakati wa mjadala uliyofanyika katika maadhimisho ya siku 16 uanaharakati dhidi ya ukatili wa kijinsia mwaka 2024.
Mjadala huo umeandaliwa na shirika sililo la kiserikali la linalojishughulisha na masuala mbalimbali ya kijamii mkoani Mtwara pamoja na mikoa mingine la TALIA kwa kushirikiana na asasi mbalimbali za kiraia pamoja na serikali, uliyofanyika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Ofisa Miradi kutoka shirika hilo, Noel Kadaga amesema lengo la mjadala huo ni kujadili kwa pamoja namna wanavyoweza kusaidiana kutoa elimu kwa jamii na kupunguza kasi ya vitendo hivyo vya ukatili vinavyotokana na changamoto mbalimbali kwenye maeneo wanayofanyia kazi.
“Tunajua kuna wahanga wa aina tofauti tofauti kama vile wa mimba na ndoa za utotoni, miradhi na ndoa,”amesema Noel.
Mjumbe kutoka jukwaa la wanawake mkoani humo, Mwanahamisi Ngomeke amesema kupitia mjadala huo viyu vingi amejifunza vitavyomsaidia kuendelea kuboresha maeneo ya utoaji wa elimu hiyo kwa jamii.

Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Mtwara, Sheikh Hassan Mpwago amesema viongozi hao wa dini kwa kushirikiana na serikali na wadau hao mbalimbali watahakikisha wanaendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya vitendo hivyo vinavyoendelea katika jamaii yao.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Ofisa Ustawi wa Jamii wa manispaa hiyo, Godlove Miho amesema jamii inapaswa kuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia.

Maadhimisho hayo yanaenda sambamba na Kauli mbiu inayosema ‘Kuelekea Miaka 30+ ya Beijing: chagua kutokomeza ukatili ya kijinsia’



