Wadau wataka elimu jumuishi kwa jamii

MTWARA: WADAU wa elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara wameliomba shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala mbalimbali ya kijamii mkoani humo (MTWANGONET) kuhakikisha elimu jumuishi inafika kikamilifu katika jamii ili ipate uelewa zaidi kuhusu mkakati wa taifa wa elimu jumuishi.

Hayo yamejiri wakati wa kikao cha tathimini ya mradi wa ‘Sauti Zetu’ unaolenga utekelezaji wa masuala ya elimu jumuishi katika jamii unaotekelezwa na shirika hilo la MTWANGONET kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo kwa sasa ni miaka miwili ya utekelezaji wa mradi, kilichofanyika kwenye manispaa ya mtwara mikindani.

Ofisa Elimu wa Elimu Maalumu Shule za Awali na Msingi wa halmashauri hiyo, Tufanye Ahmedi amesema shirika hilo limekuwa na mchango mkubwa kwenye halmashauri kwakuwa linafanya kazi kwenye shule zao,  jamii kwa ujumla kwa kutoa elimu hiyo kwa kushirikisha watu mbalimbali wakiwemo walimu wenye utaalamu wa elimu hiyo na wasiyo na utaalamu na wengine.

Aidha, halmashauri hiyo ina jumla ya shule za msingi 73 ambazo ni jumuishi kwakuwa hizo zote zina wanafunzi wenye mahitaji  na jumla ya wanafunzi wenye mahitaji ni 435 ambao wana ulemavu tofauti tofauti.

Ofisa Elimu Maalum Msingi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Bakari Ahmadi ametoa ushauri kwa shirika hilo kuwa, waweke makongamano na kuanzisha klabu za elimu jumuishi mashuleni ili watoto wote wajifunze lugha ya alama wakiwemo wenye mahitaji na wasiyo na mahitaji.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nanguruwe Imelda Kavai amelishukuru shirika hilo, ’’Elimu hii imekuwa msaada mkubwa kwangu, kabla ya elimu hii sikuwa na uelewa kuhusu elimu hii ila sasa nimepata uelewa mzuri na nashukuru pia hata jamii nayo imepata uelewa mzuri”

Ofisa mradi wa ‘Sauti Zetu’ wa taasisi hiyo na mtoa mada wa kikao hicho Deogratius Makoti alisema mradi huo ni wa miaka mitatu ambao ulianzishwa Januari 2025 na unatarajiwa kumalizika Januari 2027.

Amesema mpaka sasa ni miaka miwili ya utekelezaji wake ambao ni zaidi ya asilimia 90 na iliyobaki ni ile ya kuwafikia wanachni moja kwa moja.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button