Wadau watoa elimu nishati safi ya kupikia

ARUSHA: Wadau mbalimbali nchini wameendelea kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia.

Jitihada hizo ni pamoja na kampeni ya maonesho ya vitendo iliyofanyika jijini Arusha, ambapo wananchi wamelimishwa kuhusu matumizi ya umeme kama mbadala wa kuni na mkaa.

Warsha hizo zimeandaliwa na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa ikiwemo UKAid na Modern Energy Cooking Services (MECS) ikiwa na lengo la kupunguza utegemezi wa kuni, mkaa na gesi, ambazo husababisha changamoto za kiafya na kimazingira.

Katika maonesho hayo ya elimu ya vitendo, wananchi walijifunza kuhusu urahisi na faida za kutumia umeme kama nishati ya kupikia. Baadhi ya washiriki kama Daniel Edward na Ashura Derickvck wamesema wamehamasika kuachana na matumizi ya kuni na mkaa baada ya kushuhudia kwa macho teknolojia hiyo safi na nafuu.

SOMA ZAIDI

‘Tumeweka mikakati wananchi wote watumie nishati safi’

Mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi wa Arusha umeonesha mabadiliko ya mtazamo kuhusu nishati safi, huku wengi wao wakionesha nia ya kubadili mfumo wao wa kupikia majumbani.

Kampeni hiyo ya elimu itaendelea katika mikoa mingine nchini, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kuhakikisha Watanzania wote wanapata elimu ya matumizi salama, rafiki kwa mazingira na kuongeza matumizi ya nishati safi katika kaya kufikia asilimia 80 ifikapo 2034.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button