Wadau wawezesheni vijana wabunifu

DAR-ES-SALAAM  : WADAU wa maendeleo wametakiwa kuongeza juhudi katika kuwawezesha vijana wabunifu wanaojihusisha na biashara ndogo na za kati, ili kuchangia ustawi endelevu wa jamii.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Afisa Programu wa Ubalozi wa Uswisi, Daniella Kwayu, katika mkutano uliowakutanisha wawekezaji na vijana wafanyabiashara wa biashara bunifu.

“Mkutano huu umekusanya wawekezaji na wafanyabiashara wachanga wanaoendesha shughuli zenye manufaa kwa mazingira na jamii, huku zikiwa endelevu na kuongeza ajira kwa vijana,” alisema Kwayu.

Kwa upande wake, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Nicole Providoli, alisema taifa lake linaendeleza ushirikiano na Tanzania katika kusaidia miradi ya kuwawezesha vijana wabunifu.

SOMA:  SBL yawawezesha wanawake, vijana katika ujasiriamali

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button