SBL yawawezesha wanawake, vijana katika ujasiriamali

MWANZA: Katika eneo la Kanda ya Ziwa nchini Tanzania, mjasiriamali kijana anahesabu kwa makini mapato ya siku nyuma ya kaunta yake. Mwaka mmoja uliopita, suala la kusimamia fedha na hesabu za bidhaa lilimshinda. Sasa anaendesha biashara yake kwa ujasiri, akijijengea njia ya kuelekea kwenye ukuaji endelevu. Mabadiliko yake ni ushahidi wa mabadiliko chanya kupitia mpango wa Learning for Life wa Serengeti Breweries Limited (SBL)—mpango kabambe kwa wale wanaotafuta ajira katika sekta ya ukarimu, lakini wamekumbwa na changamoto za kielimu au ajira.

SBL, kama moja ya kampuni zinazoongoza kwa uzalishaji wa vinywaji nchini Tanzania, imejikita kwa muda mrefu katika kuwezesha kiuchumi wanawake na vijana wajasiriamali. Kupitia mpango huu wa Learning for Life, SBL inavunja vizingiti vya utegemezi kwa kuwapatia washiriki mafunzo muhimu ya ujuzi wa biashara, elimu ya fedha, usimamizi wa mikopo na hatari, udhibiti wa bidhaa, pamoja na kukuza uongozi.

Awamu ya hivi karibuni ya mpango huu, iliyoanzishwa Kanda ya Ziwa kwa ushirikiano na Bridge for Change (BFC), tayari inabadilisha maisha ya wanawake wauzaji wa bidhaa 50. Lengo si tu kuwawezesha kustahimili changamoto za soko bali kuwapa nguvu za kufanikiwa na kustawi.

Kwa wanawake na vijana wengi, fursa ya kupata mafunzo na ushauri ni ya kubadilisha maisha. Magreth John, mmoja wa walionufaika na mpango huu, anakumbuka changamoto alizokutana nazo kabla ya kujiunga.

“Kabla ya mafunzo haya, nilikuwa napata shida kusimamia bidhaa zangu na kuweka rekodi za kifedha. Mafunzo yamenifumbua macho kuhusu upangaji bora wa fedha, na sasa nafanya maamuzi ya busara yanayosaidia biashara yangu kukua. Nina ujasiri wa kuongeza bidhaa na hata kumuajiri mfanyakazi wa kusaidia shughuli zangu.”

Sarah Modesto, muuzaji wa bidhaa kutoka Shinyanga, anasimulia uzoefu wake pia:

“Nimejifunza namna ya kusimamia fedha, kuweka kumbukumbu sahihi za biashara, na kukuza mtaji wangu huku nikipunguza matumizi yasiyo ya lazima. Mafunzo haya yamenipa mtazamo mpya juu ya kuendesha biashara kwa ufanisi na kujiamini zaidi.”

Kwa wajasiriamali wengi, ukuaji wa biashara hauhusiani tu na kuongeza mauzo—bali na kujifunza misingi ya usimamizi wa fedha na uendelevu.

Serikali ya Tanzania imekuwa ikihamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uchumi, na mpango wa Learning for Life unachangia moja kwa moja juhudi hizi kwa kuwapatia mafunzo ya vitendo, yakiwemo maarifa ya kifedha na usimamizi wa hatari, yanayowawezesha kufanya maamuzi sahihi ya biashara na kuongeza ajira kwenye jamii zao.

Dorice Swai, muuzaji wa bidhaa kutoka Musoma, anaeleza jinsi mafunzo haya yalivyobadilisha namna anavyosimamia biashara yake:

“Hapo awali, sikuwa ninaelewa wa kina juu ya umuhimu wa kuweka kumbukumbu na kufuata taratibu za kodi, lakini sasa najua jinsi ya kufanya hayo kwa usahihi na kushirikiana vizuri na TRA. Pia nimepata ujuzi wa kusimamia biashara kwa ufanisi, jambo linalohakikisha ukuaji endelevu.”

Mbali na kuweka kumbukumbu, washiriki wa mafunzo haya wanajifunza pia namna ya kuweka bei shindani lakini zenye faida changamoto kubwa kwa wamiliki wa biashara ndogo. Theresia Emmanuel, muuzaji wa bidhaa kutoka Tabora, anaelezea jinsi mafunzo haya yalivyomsaidia kushinda changamoto za bei na usimamizi wa hatari:

“Kabla ya mafunzo haya, mara nyingi nilikuwa naogopa kuweka bei ya juu kwa kuhofia kupoteza wateja, hali iliyopunguza faida zangu. Kupitia mafunzo ya Learning for Life, nimejifunza kuweka bei shindani lakini zenye faida. Sasa ninaelewa mbinu za kudhibiti hatari zinazoweza kujitokeza katika biashara. Maarifa haya yamenipa ujasiri wa kufanya maamuzi sahihi na kukuza biashara yangu kwa njia endelevu.”

Mpango wa Learning for Life wa SBL si tu mpango wa kukuza ujuzi wa biashara ni kichocheo cha ujumuishaji wa kifedha. Kwa kuwasaidia washiriki kusajili biashara zao rasmi na kupata huduma za kifedha na mikopo, mpango huu unawafungulia njia ya kupanua biashara na kuimarisha mafanikio ya muda mrefu.

SBL yawanoa wanawake, vijana wanaosambaza vinywaji

Kwa mujibu wa Gordon Katundu, Meneja Mauzo wa wa SBL Kanda ya Mwanza, maendeleo ya kweli hupimwa kwa fursa zinazotengenezwa kwa jamii:

“Kupitia mpango wa Learning for Life, hatuwekezi tu kwenye ujuzi wa biashara tunawekeza kwa watu. Kwa kuwawezesha wanawake na vijana kwa nyenzo za kuendesha biashara zenye mafanikio, tunachochea uhuru wa kiuchumi na uendelevu wa muda mrefu.”

Biashara zinapozidi kustawi, zinachangia kwenye uchumi wa maeneo yao, kuongeza ushindani wa kimasoko, na kuleta ubunifu—huku zikiimarisha mfumo wa biashara nchini Tanzania.

Athari ya SBL katika kuwezesha kiuchumi haijabaki kuwa ya muda mfupi. Kupitia mpango wake wa Learning for Life, kampuni inaendelea kutoa ushauri na msaada wa kudumu, kuhakikisha wajasiriamali wanatumia ipasavyo maarifa waliyojifunza. Kwa kuimarisha ushirikiano na taasisi kama BFC, SBL inapanua mafunzo haya hadi mikoa mingine, ikikuza usawa na ujumuishaji, kuhakikisha wanawake na vijana wengi zaidi wanapata fursa za kiuchumi.

Mafanikio ya mpango wa Learning for Life yanadhihirisha kuwa kampuni zinapowekeza kwa watu, athari yake haibaki kwa mtu mmoja tuinabadilisha jamii nzima. Kadri mazingira ya ujasiriamali yanavyoendelea kubadilika nchini Tanzania, mahitaji ya mafunzo, ushauri, na ujumuishaji wa kifedha yanaendelea kuwa muhimu.

Mpango huu wa SBL unafungua njia kwa mustakabali ambapo wanawake na vijana hawatakiwi tu kustahimili bali wanapaswa kustawi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button