Waendesha baiskeli waandaa tamasha la muziki Butiama

ARUSHA: WAENDESHA baiskeli Twende ‘Butiama Cycling Your’ wameandaa tamasha maalumu la muziki jijini Arusha kwa ajili ya kuhamasisha utunzaji wa ikolojia ya Mlima Kilimanjaro

Miti zaidi ya 50,000 inatarajia kupandwa katika kampeni ya Twende Butiama katika kuhakikisha wanamuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika kuelekea kilele cha kuzaliwa kwake.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuandaa tamasha maalumu la kusaidia jamii mbalimbali ikiwemo utunzaj wa mazingira, Mkuu wa Uhusiano na Vyombo vya Habari kutoka Vodacom Tanzania, Annette Kanora amesema kampeni ya Twende Butiama imeshaanza kwa kufanya mambo mbalimbali huku kilele chake kikiwa ni Oktoba 14 mwaka huu ingawa ni mwaka wa uchaguzi wameanza sharamshara hivi sasa.

Amesema waendesha baiskeli hao walianza mbio hizo Julai mwaka huu na kulala Mkata Handeni mkoani Tanga kisha wakaendelea na safari hadi Hedaru mkoani Kilimanjaro na kufikia mkoani Arusha.

“Wanaendelea na safari yao na wanatarajia kufika Butiama Oktoba 13 mwaka huu na mwaka jana madawati zaidi ya 1,100 yalichangwa katika shule za msingi 11”

Naye, Kiongozi wa Msafara wa Twende Butiama, Gabriel Landa  amesema msafara huo wa baiskeli unalengo la kumuenzi Hayati Baba wa Taifa, Nyerere ambapo msafari huo ulianza mwaka 2019 kwalengo la kuibua hisia kwa waendesha baiskeli dhidi ya kuenzi shughuli mbalimbali alizokuwa akizifanya ikiwemo kuhammsisha amani ikiwemo mapambano ya ujinga, umaskini na maradhi.

“Tunachangishana kwaajili ya kuchangaia madawati, mazingira kwa upandaji miti na kwa upande wa marathi tunahamasisha zaidi watanzania kufanya mazoezi ili kuondokana na tabia bwete”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button