Wafanyabiashara Kagera kusikilizwa changamoto zao

KAMISHNA wa Mamlaka ya Mapato (TRA),  Yusuph Mwenda amewahakikishia wafanyabiashara mkoani Kagera kuwa atamtuma kamishina wa kodi za ndani kabla ya Oktoba mwaka huu ili kusikiliza kero na changamoto zao.

Kamishina huyo amefanya ziara ya kikazi mkoani Kagera ya kukutana na wafanyabiashara ambapo amemwaagiza meneja wa TRA Mkoa wa Kagera kuandaa orodha ya majina ya wafanyabiashara ambao wanakumbwa na madeni ya nyuma ambao walifunga biashara zao na baadhi wameamua kurejea upya katika biashara hizo huku wengine wakiendelea kukumbushia ahadi ya Rais ambayo alitoa ufafanuzi kuhusu kufutwa kwa madeni hayo ya nyuma

“Nimepokea maoni ya wafanyabiashara Kagera kuhusu ,swala ambalo lilitolewa maelekezo na Raisi wa jamuhuru ya muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu alipofanya ziara mkoani Kagera July 2022 na kuagiza kuwa Madeni hayo yafutwe na wafanyabisha waliokimbia Biashara zao warudi TRA kuanza upya na kufanya biashara nisema kuwa kabla ya Oktoba mwaka huu kamishina wa mapato ya ndani atawasilikiza na hii changamoto itatatuliwa mara moja na tutaendelea kushirikiana katika maswala ya kuuza uchumi wetu,” alisema Mwenda.

Maswala mengine ambayo amewahaidi wafanyabiashara mkoani Kagera ni kuwa TRA itaendelea kupunguza vikwazo kandamizi katika mipaka iliyoko mkoa wa Kagera ambavyo vinakwamisha biashara, pamoja na kuwahakikishia kuwa watumishi wa makulaka hiyo wataendelea na utamaduni wa kuwatembelea katika biashara zao ili kuwasikiliza na kutafuta changamoto za kibiashara.

Baadhi ya Wafanyabiashara na wajasiriamali mkoani Kagera walioudhuria mkutano huo ,pamoja na kutaka mamulaka hiyo kutatua changamoto ya madeni ya nyuma pia wameitaka mamlaka ya mapato nchini TRA ,kutoa elimu ya mara kwa mara juu ya umuhimu na taratibu za ulipaji kodi ili kuondoa sintofahamu za mara kwa mara baina ya mamlaka hiyo na wafanyabiashara hao.

Silvanus Joseph Mfanyabiashara amesema kuwa kuna mabadiliko makubwa ambayo yamekuwa yakifanyika baina wafanyabiashara na watumishi wa TRA huku akidai kuwa kama maagizo ya Rais yatafanyiwa kazi basi wafanyabishara watakuwa wamefufua matumaini yao mapya na watahamasika zaidi kulipa kodi mapato yataongezeka huku akipongeza mabadiliko makubwa yanayofanywa na serikali katika kuhakikisha wanawekewa mazingira rafiki ya kulipa Kodi.

Nicholaus Basimaki, Mwenyekiti Jumuiya ya wafanyabiashara (JWT) Mkoa Kagera na Kanda ya Ziwa amesema Rais alipotoa tamko la wafanyabishara wenye madeni ya miaka ya nyuma ambao walipitia changamotoo kufutiwa kodi na kuanza upya ilileta amani na utulivu.

Amesema kutotekelezeka kwa agizo hilo kumegeuka mwiba kwa wafanyabishara hao na baadhi wanakaribia kuukimbia tena mkoa huo na kusitisha biashara zao ambapo amemuomba kumsisitiza kamishna kushughulikia swala hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button