Wafanyabiashara madini wakumbushwa sheria

DODOMA: Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ametoa rai kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuzingatia sheria zilizowekwa ili kuhakikisha sekta hiyo inaendeshwa kwa uadilifu na manufaa kwa taifa.

‎Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Waziri Mavunde amesema Serikali haitavumilia uvunjifu wa sheria unaosababisha upotevu wa rasilimali za taifa.

‎Akizungumza kuhusu hali ya biashara ya madini, Waziri Mavunde amesema wizara yake imeendelea kuchukua hatua kudhibiti utoroshaji madini kwa baadhi ya wachimbaji na wafanyabiashara wasio waaminifu.

‎Aidha, amebainisha  kuwa mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umekuwa ukiimarika mwaka hadi mwaka ambapo uliongezeka kutoka asilimia 9.1 mwaka 2023 na kufikia asilimia 10.1 mwaka 2024, hadi kufikia kipindi cha robo tatu ya mwaka 2025 (Januari – Septemba) wastani wa mchango

‎wa sekta umefikia asilimia 11.9.‎Hata hivyo Waziri Mavunde amesema Mwenendo huu umechangiwa na kuongezeka kwa uwekezaji katika Sekta ya Madini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button