Wafanyakazi wapewa mbinu za kunufaika na mifuko mbalimbali

WAFANYAKAZI kutoka maeneo mbalimbali wameshauriwa kuwa na utaratibu wa kuhudhuria semina za mara kwa mara zitakazowasaidia kujua haki na manufaa ya kuwa kwenye vyama  vya Wafanyakazi.

Hayo yamesemwa leo Agosti 25, 2023 katika semina iliyokutanisha Wafanyakazi kutoka matawi mbalimbali  Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, ambapo katibu Mkuu Chama za wafanyakazi wa Taasisi za Juu (RAAWU) Joseph Sayo amesema semina hizo zinawasaidia Wafanyakazi kujua mambo mbalimbali yanayojitokeza kwenye mifuko ya Wafanyakazi ili kwenda sambamba na matakwa yao.

Katika hatua nyingine mwanachama wa RAAWU kutoka Zanzibar Dk Mohamed kombo Maalim amesema semina hizo zinawasadia Wafanyakazi kujua mambo muhimu wanayopaswa kufanya wakiwa Watumishi.

kwa upande wao Wafanyakazi wengine wa ambao ni wanachama wa RAAWU wanasema elimu waliyopatiwa itawasaidia katika kuyaendea mambo mbalimbali yanayowahusu wafanyakazi na kuwa mabalozi wazuri kwa wengine.

Habari Zifananazo

Back to top button