Wafungwa 1700 waachiwa huru

UINGEREZA : ZAIDI ya wafungwa 1,700 nchini Uingereza na Wales wataachiliwa huru mapema hii leo, kama sehemu ya mpango wa serikali ulioundwa wa kupunguza msongamano magerezani.
Hatua hiyo ilichochewa na serikali ya Labour iliyoingia madarakani siku chache baada ya uchaguzi mkuu mwezi Julai, lakini maafisa walikuwa tayari wameshapanga wakati chama cha Conservative kikiwa bado madarakani.
Sera hiyo itawaruhusu wafungwa kuachiliwa baada ya kukamilisha 40% ya kifungo chao – badala ya 50% – katika jitihada za kuhakikisha vitanda 5,500 vinakuwa wazi.
soma : Huruma ya Rais Magufuli kwa wafungwa, asamehe waliopaswa kunyongwa
Lakini sera hiyo haitatumika kwa wafungwa waliopatikana na hatia ya makosa ya ngono, ugaidi, unyanyasaji wa nyumbani au baadhi ya makosa ya vurugu.
SOMA : Kampeni ya Mama Samia yawatoa wafungwa, mahabusu 7000



