Wagombea 8 UWT kuchuana Kagera

KAGERA: WAJUMBE wa Mkutano Mkuu kutoka Wanawake Mkoa wa Kagera (UWT) wameelezwa kwamba baada ya uchaguzi wa kupata wagombea wawili watakaowania nafasi ya Viti Maalumu, wanachama wote waendeleze mshikamano ili kutekelza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwenyekiti wa Uchaguzi, Hajath Faidhah Kainamura ambaye ndiye Mwenyekiti wa UWT wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu UWT mkoani Kagera amesema kuwa ni muda wa kuwachagua wawakilishi na baada ya hapo wanachama wanapaswa kushikamana ili kukomboa kura za uraisi ubunge na udiwani.
Amesema katika zoezi la kupata mgombea yapo mambo ya kupata na kukosa kuchaguliwa mambo yanayotakiwa kufanya ni kushikamana ili kuleta maendeleo mazuri ndani ya chama.

“Tuondoe chuki, baada ya uchaguzi kinachotakiwa katika chama ni mshikamano wenye kutenda,utekelezaji na kupata mafanikio mazuri tanayoleta maendeleo,” amesema Kainamura
Katibu wa umoja wa wanawake mkoa wa Kagera UWT Rehema Zuberi amesema awali watia nia wa nafasi wa viti Maalumu walijitokeza wakiwa 13 mmoja kati yao hakuweza kurudisha fomu.
Aidha, majina yalipelekwa kamati kuu ili iweze kufanya uchaguzi wa majina baada ya kukamilisha iliweza kurudisha wagombea nane ambao ndio wanapigiwa kura na na wajumbe na wagombea wanne wamerudishwa majina yao huku akidai kuwa wajumbe wanaopiga kura kwa wajumbe ni 1,556
Msimamizi wa Uchaguzi Yassim Bachu ambaye ni Msimamizi Baraza kuu la utekelezaji Taifa amesema kuwa, wajumbe wanatakiwa kupiga kura kwa umakini na kutovunja sheria za uchaguzia na badala yake wachague kwa haki ili kupata wawakilishi wazuri watakaotambua mahitaji yao.

