Wagombea Morogoro washukuru kwa maendeleo majimboni

MOROGORO: WAGOMBEA Ubunge wa Majimbo ya Kilosa, Mvomero na Mikumi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka maendeleo katika majimbo yao.

Mgombea wa Jimbo la Kilosa, Profesa Palamagamba Kabudi alisema serikali imetekeleza ahadi zake za kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga shule za sekondari na msingi katika kata zote za jimbo hilo. Serikali pia, imetoa zaidi ya Sh bilioni 700 katika ujenzi wa barabara na madaraja na kuimarisha mawasiliano kwa kujenga minara 21 ya mawasiliano.

Alimshukuru Rais Samia kwa kukamilisha ujenzi wa barabara yenye urefu kilometa 25 iliyochukua miaka 20 hadi kukamilika kwake katika awamu hii na kusisitiza kuwa sasa safari ya ujenzi wa barabara ya Kilosa- Mikumi imeanza. SOMA: SUA yapata miradi ya utafiti ya bil 3.8/-

Naye mgombea wa Jimbo la Mikumi, Dennis Londo alisema Rais Samia amefanya mapinduzi makubwa katika jimbo hilo iliyoacha alama ya kudumu. Alisema uwepo wa Reli ya Kisasa (SGR) imefungua milango ya uwekezaji na wawekezaji wanaendelea kujitokeza kwa wingi na kupandisha thamani ya ardhi ya Kilosa.

Londo alisema kupitia filamu ya Tanzania: The Royal Tour, idadi ya watalii imeongezeka kufikia 1,300 katika Mbuga ya Taifa ya Mikumi na kutoa ajira kwa vijana, mamalishe na waongoza watalii. Kwa upande wa mgombea wa Jimbo la Mvomero, Sara Msafiri alisema kupitia kampeni ya Tutunzane iliyoanzishwa na Rais Samia na kusimamiwa na viongozi wa kimila na wa dini, imesaidia kumaliza migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika jimbo la Mvomero.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button