Wagombea wagomea mdahalo wa rais Senegal

WAGOMBEA wengi katika uchaguzi wa rais uliocheleweshwa nchini Senegal wamesema hawatashiriki katika mdahalo wa kitaifa uliopendekezwa na Rais Macky Sall.

Jumla ya wagombea 16 kati ya 19 wanaokataa mazungumzo hayo.

Siku ya Alhamisi, Sall aliahidi kuachia ngazi ifikapo Aprili 2, 2024 2 lakini alishindwa kupanga tarehe ya kuchaguliwa kwa mrithi wake.

Kundi hilo lilitaka uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe hiyo.

“Tunatoa wito wa kuhamasishwa,” mgombea urais Aliou Mamadou Dia alisema, akiongeza kuwa kundi hilo lilikuwa likifanyia kazi mpango wa utekelezaji utakaofanyika Jumatatu na Jumanne.

Habari Zifananazo

Back to top button