Wahamiaji haramu mbaroni wakijifanya wachezaji Coastal

JESHI la Uhamiaji Mkoa wa Tanga, limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu wanne raia wa Cameroon, ambao wamedai wapo nchini  kwa ajili ya kufanya majaribio ya  kujiunga na timu za Coastal Union na African Sports zilizopo jijini Tanga.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Kagimbo Bakari amesema wahamiaji haramu hao wamedai wameletwa na wakala aitwaye Benard Matomondo Mfaume na kwamba waliingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA) na kupata visa ya matembezi (HV) za siku 90, badala ya visa za kibiashara (BV) kulingana na shughuli walizokuja kuzifanya.

Hata hivyo alibainisha kuwa mara baada  ya kuwakamata raia hao, waliwaita viongozi wa timu za African Sports na Coastal, ambao walikana kuwatambua wala kuwa na mawasiliano nao na barua walizokuwa nazo zote ni za kughushi na pasipoti walizokuwa nazo sio sahihi.

Habari Zifananazo

Back to top button