UGIRIKI : WAHAMIAJI watatu wamekufa na wengine takriban 25 hawajulikani walipo baada ya mashua yao kuzama hii leo karibu na kisiwa cha Ugiriki cha Samos.
Wakizungumzia kuhusu tukio hilo , baadhi ya walinzi wa eneo hilo wamesema wamefanikiwa kuwaokoa wahamiaji watano wakati shughuli ya utafutaji na uokoaji ikiendelea kwa kutumia meli nne na helikopta huko Agios Isidoros kaskazini-magharibi mwa kisiwa hicho.
Kati ya mwaka 2015 hadi 2016, Ugiriki ilikuwa lango kuu la wahamiaji kutoka Mashariki ya Kati, Afrika na Asia kuingia barani Ulaya, ambapo karibu watu milioni 1 waliwasili kwenye visiwa vya nchi hiyo kwa kutumia mashua.
Hatahivyo ongezeko la wahamiaji lilishuka miaka ya nyuma lakini mwaka jana idadi ikaanza kuongezeka nchini humo .