Wahusika LBL Dar wanaswa

DAR ES SALAAM: JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa 26 wahusika wa Kampuni ya Leo Burnett London (LBL) kwa tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya kuendesha upatu mtandaoni bila kuwa na kibali cha Banki Kuu ya Tanzania.
Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 24, 2024 na jeshi hilo imeeleza kwa kushirikiana na Benki Kuu walifanya uchunguzi katika kampuni hiyo na kubaini haina uongozi maalumu na ufanyaji kazi wake ni lazima uanze kwa kutoa pesa ili uwe mwanachama.
Soma zaidi: Meneja LBL anaswa biashara ya upatu mitandaoni
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kampuni hiyo huchangisha pesa kwa kuwadanganya wananchi kuwa watapata faida kubwa kwa muda mfupi.
Jeshi hilo la polisi limesema upelelezi utakapokamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazowakabili huku likitoa wito kwa wananchi wote kuacha kujihusisha na biashara za upatu mitandaoni bila kujiridhisha ka kuwa baadhi ya biashara hizo hazina leseni wala vibali kutoka katika mamlaka husika za kisheria.
Soma zaidi: JESHI la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia watuhumiwa …



