Wajadili changamoto na huduma kwa wafanyabiashara

WAKUU wa taasisi mbalimbali za serikali nchini pamoja na za  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, leo Januari 6, 2023 wamekutana kwenye kongamano la 9 la Biashara Zanzibar na kufanyanya mazungumzo yaliyolenga kuendeleza ushirikiano katika kutatua changamoto na kuboresha huduma kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili.

Akizungumza katika kongamano hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar,  Rashid Salim amesema kuna changamoto ambazo zinaweza kutatuliwa, endapo taasisi hizo zitashirikiana kupeana taarifa, kufanya mafunzo ya pamoja, kushiriki mikutano na kushirikiana kuandaa miradi.

Amesema kongamano hilo ni hatua muhimu katika kudumisha Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana katika kuhahikisha taasisi hizo zinawawezesha wafanyabiashara nchini.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade),  Latifa Khamis amesema kongamano hilo limewaleta pamoja wakuu wa taasisi na kujadiliana mada zilizolenga kutatua changamoto katika usajili wa biashara na leseni, ushindani na halali, viwango na vipimo, viwanda na biashara.

Baadhi ya taasisi zilizoshiriki ni  BRELA, TANTRADE, TBA, ZAWEMA, ZAEA,BLRC, SMIDA,TIRDO, SIDO, TIRA na  WRRB.

 

Habari Zifananazo

Back to top button