Wajasiriamali washauriwa kutumia fursa soko EAC

KAIMU Katibu wa Wajasiriamali Taifa na Mwenyekiti wa Wajasiriamali Wanawake Mkoa wa Arusha, Husna Almasy amewataka wajasiriamali nchini kuchangamkia soko la pamoja la bidhaa kwenye nchi za  Jumuiya ya  Afrika Mashariki (EAC)

Husna ametoa rai hiyo wakati alipozungumzia umuhimu wa nchi nane za EAC na fursa za biashara kwa wajasiriamali nchini Tanzanii kwenda katika nchi za EAC.

Advertisement

Ameishukuru serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Hassan Suluhu ya kuifungua Tanzania katika soko la pamoja la bidhaa ambalo linatoa fursa kwa wajasiriamali kuuza bidhaa zao wanazozalisha katika nchi hizo

Amesema hata katika kikao cha wakuu wa nchi kilichofanyika jijini Arusha wiki iliyopita wajasiamali kutoka nchi mbalimbali za jumuiya na wa Mkoa wa Arusha wameuza bidhaa zao ikiwemo kupata masoko katika nchi nyingine.

“Nawasihi wajasiamali wenzangu zinapotokea fursa tujitokeze kuzisaka milango ya biashara ipo wazi tutumie zaidi mitandao ya kijamii kwaajili ya kutangaza bidhaa zetu tuweke na mawasiliano yetu hivi sasa biashara za mtandao ni kubwa hivyo tutumie teknolojia hii kuuza bidhaa zetu katika nchi za EAC na kimataifa na tuhakikishe zinaubora na kuweka alama zetu wanunuzi wajue zimetoka Tanzania”

Wakati huo huo, Husna amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mkoa, Paul Makonda kwa ubunifu wake na kuwajali wajasiamali wadogo kwa kuuza bidhaa zao kwenye mikutano mbalimbali ikiwemo matamasha ikiwemo tamasha la Land Rover Festival lilofana zaidi.