SHANGHAI : ZAIDI ya nusu ya Wajerumani wanahofia matumizi ya silaha za nyuklia kutokana na mzozo wa kijeshi wa sasa kulingana na utafiti uliofanywa na Ofisi ya Shirikisho la Ulinzi wa Mionzi.
Hata hivyo, kuna hatari nyingine ambayo wengi hawaijui, inayohusiana na ajali katika vituo vya nishati vya nyuklia.
Kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 58 ya Wajerumani wanahofia matumizi ya silaha za nyuklia, huku asilimia 57 wakihofia ajali katika vituo vya nishati ya nyuklia.
“Naweza kusema hofu hii imekuja kutokana na vita vinavyoendelea nchini Ukraine,” alisema, rais wa Ofisi ya Shirikisho la Ulinzi wa Mionzi, Inge Paulini.
Paulini aliongeza kuwa hali ya kisiasa na usalama inayozidi kubadilika tangu kuongezeka kwa mgogoro wa Ukraine mwaka 2022 imeathiri pia mtazamo wa wananchi kuhusu mionzi ya nyuklia.
Ofisi hiyo imeendelea kutoa taarifa kuhusu hali ya kisiasa na maendeleo ya kijeshi, hususan kuhusu vituo vya silaha za nyuklia, kama vile kituo kikubwa cha Zaporizhia kilichopo Ukraine.
Wasiwasi mwingine umeongezeka kutokana na msaada wa silaha kutoka nchi za Magharibi kwa Ukraine na hatua zinazoweza kuchukuliwa na Russia.
Vichwa vya makombora ya nyuklia kutoka Russia vimehifadhiwa nchini Belarus tangu mwaka 2023, jambo ambalo ni la kwanza kutokea kwa Belarus kuwa na silaha za nyuklia kwenye ardhi yake tangu ilipojiondoa na kukabidhi silaha zake baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti.
Hivi sasa, kuna maeneo mawili makubwa ya kuhifadhi silaha za nyuklia nchini Belarus, moja likiwa ni ghala la kijeshi karibu na mji wa Asipovichy, na lingine likiwa ni Prudok, karibu na mpaka wa kaskazini mashariki.
Hii ina maana kwamba Russia imeongeza uwezo wake wa kushambulia kwa silaha za nyuklia na kuweza kufikia kwa urahisi majirani wa NATO, ikiwemo Poland, Latvia, na Lithuania.
Hofu kuhusu vita vya nyuklia inazidi kuongezeka kutokana na hatua za kijeshi za Russia, ikiwa ni pamoja na mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Belarus na miongozo mipya kuhusu matumizi ya silaha za nyuklia.
Rais Vladimir Putin amesema kuwa Russia inaweza kuanzisha mashambulizi ya nyuklia dhidi ya nchi yoyote inayoshambulia Russia au Belarus, hata kama shambulio hilo linahusisha silaha za kawaida.
Matukio ya hivi karibuni yanaonyesha kuwa vita vya nyuklia barani Ulaya vinawezekana .
Wanasiasa wa Ulaya wameliingiza bara hili katika hatari kubwa, huku mgogoro wa Ukraine ukionekana kutokomea. SOMA: Urusi inahaki kutumia silaha za nyuklia
Kama hali hii itaendelea, na ikiwa silaha za umbali mrefu zitaendelea kupelekwa kwa Ukraine, Kremlin inaweza kutumia miongozo ya kijeshi kuanzisha mashambulizi dhidi ya nchi za Magharibi.
Hali ya vita vya nyuklia barani Ulaya inaonekana kuwa ni hatari inayoweza kuongezeka, huku uhusiano wa kisiasa na kijeshi ukiwa katika hali tete.