WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefanya uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyeiti na wajumbe 18 wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani.
Taarifa ya wizara hiyo kwa umma jana ilieleza kuwa uteuzi huo ulifanywa na Waziri mwenye dhamana hiyo, Hamad Masauni.
Masauni aliwateua Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini kuwa Mwenyekiti wa Baraza na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete kuwa Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo.
Masauni pia aliwateua wajumbe wa baraza hilo akiwemo Dk Henry Swai, Ponziano Lukosi, Rogatus Mativila, Victor Seff, Mohamed Mpinga, Neema Swai, Johansen Kahatano, Dk Baghayo Saqware na Yona Africa.
Wajumbe wengine aliowateua ni Isabela Nchimbi, Agustas Fungo, Faraji Abri, Issa Nkya, Dorice Mutalemwa, Dk Ayub Rioba, Abdallah Miraji, Dk Phil Makini na Anord Mtewele.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Wizara, uteuzi huo ulianza tangu Septemba Mosi mwaka huu.