Wakazi wa Pemba dumisheni amani

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika futari ya pamoja aliyowaandalia.
Hafla hiyo imefanyika leo, tarehe 12 Machi 2026, katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi uliopo Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, na imehudhuriwa pia na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi. SOMA: Dk Mwinyi aanika mafanikio lukuki afya, amani, Muungano

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Dk. Mwinyi amewaomba wananchi kuendelea kuwaombea dua viongozi wakuu wa nchi ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kukabiliana na changamoto zinazojitokeza, hasa katika ulimwengu wa sasa unaokabiliwa na majanga mbalimbali yanayotishia amani ya dunia.
Aidha amesisitiza umuhimu wa kuiombea nchi ili iendelee kudumisha amani na utulivu. Futari hiyo imewakutanisha watu wa makundi mbalimbali, wakiwemo mayatima, wajane, watu wenye ulemavu, walimu wa madrasa, masheikh pamoja na maimamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.



