Wakili ajitosa ubunge Kalambo

RUKWA: WAKILI Fortunatus Sichone ,45, ametangaza nia yake ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kalambo lililopo mkoani Rukwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi Mkuu.

Kwa sasa mbunge wa jimbo hilo ni Josephat Kandege.

Sichone ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa kupitia Jumuiya ya Wazazi amesema ameamua kugombea ubunge jimbo hilo baada ya kuona hali ya maendeleo hafifu kwa miongo kadhaa.

“Nimekuwa na ndoto ya kuwakilisha wananchi bungeni tangu nikiwa mtoto miaka 30 iliyopita …. Jimbo la Kalambo lina changamoto kadhaa kubwa ni migogoro ya ardhi imekuwepo tangu nikiwa mdogo hadi sasa,” amesema.

Akizungumza na mtandao wa HabariLEO wakili huyo amesema wakati ukifika atachukua na kujaza fomu za kugombea ubunge akisisitiza kuwa atatumia taaluma yake ya sheria kusaidia kusuluhisha migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi wa jimbo hilo kwa miaka mingi.

Aidha, amewataka Watanzania wenye sifa washiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika baadae mwaka huu ikiwa ni haki yao kikatiba.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button