Wakili Mndeme ataja vipaumbele vitatu Kigamboni

DAR ES SALAAM: MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kigamboni, jijini Dar es Salaam kupitia Chama cha ACT – Wazalendo, Wakili Mwanaisha Mndeme ameahidi kutatua changamoto ya barabara, upatikanaji wa vivuko kwa hei nafuu, na kuondoa malipo Daraja la Nyerere.
Wakili Mndeme ametoa ahadi hiyo leo Septemba 6, 2025 wakati akinadi sera zake viwanja vya Maganila kata ya Tungi Kigamboni, huku akitaja vipaumbele vitatu tajwa hapo juu.

Akichambua namna ya kutatua changamoto hizo mbele ya wananchi wa Kigamboni, Wakili Mndeme amesema atahakikisha kunakuwa na uhakika wa vivuko na vya bei nzuri.
“Tulikuwa na MV Magogoni, MV Kazi na MV Kigamboni kivuko cha MV Magogoni kipo matengenezo tangu 2023 leo ni 2025 wanasema matengenezo yamefikia asilimia 55%,MV kigamboni kimetengnezwa kwa asilimia 10% tu ina maana tuna miaka mingine takribani saba kivuko kiweze kutengenezwa. CCM imeshindwa kuhakikisha tuna uhakika wa vivuko”

Pia ameahidi kuondoa malipo kwenye daraja la Mwalimu Nyerere (maarufu kama Daraja la Kigamboni) akieleza kuwa atafuatilia kufahamu ni deni kiasi gani NSSF bado inadai kutokana na zile asilimia 60% iliyozitoa katika ujenzi wa daraja hilo ili kujua kama limeisha basi wananchi waweze kupita bila kulipia gharama.
“Tunafahamu moja ya changamoto Wanakigamboni wanapata nayo shida ni daraja la Mwalimu Nyerere ndiyo daraja pekee ambalo linalipiwa katika nchi yetu,lakini suala la kulipia daraja imekuwa ni mzigo kwa wana-Kigamboni tunafahamu liljengwa kwa bilioni mia mbili kumi na tatup kwa ubia (NSSF aslimia 60% serikali 40%) hatuna taarifa huo mkopo ambao NSSF ilichangia daraja imebaki kiasi gani,” amehoji Mndeme.



