Wakuliwa wa kahawa Kagera washusha pumzi

MKUU wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa amewahakikishia wakulima wa kahawa mkoani humo kuwa wataendelea kupata bei nzuri ya kahawa na kulipwa fedha pale wanapouza kahawa ndani ya saa 24.

Hatua hiyo ni baada ya vyama vya ushirika kuonyesha ushindani wa kukusanya kahawa ya wakulima na kuiuza bei sawa na watu binafsi wanaonunua kahawa kutoka nje ya nchi.

Mwasa aliyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa vyama vya ushirika mkoani Kagera katika jukwaa la maendeleo ya ushirika ambalo limefanyika kwa mara ya kwanza mkoani Kagera lenye lengo la kuimarisha umoja wa vyama vya ushirika.

Alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha mkulima ananufaika na kilimo anachokifanya huku akipongeza juhudi za vyama vya ushirika katika kuhakikisha wanashirikiana na Bodi ya Kahawa kuuza kahawa ya mkulima kupitia mnada na mkulima huyo akapata Bei nzuri Jambo ambalo linaongeza hamasa ya wakazi wa mkoa wa Kagera kulima zaidi.

“Visa vya utoroshaji wa kahawa vimepungua wakulima wanachohitaji nibei nzuri , ukinunua kahawa yao kwa bei nzuri hata utoroshaji wa kahawa hautafanyika ,zamani nchi jirani ndo walisifika kuwa na Bei nzuri lakini kwa Sasa vyama vyetu vikuu vya ushirika kupitia Amcos zetu ndo vinatoa bei nzuri kwa wakulima hili ni jambo linalotoa faraja Sana ,tusikubari Kurudi tulikotoka ,tushirikiane na serikali kurudisha Furaha ya mkulima wa Kagera”alisema Mwasa.

Aidha aliwaagiza wakuu wa wilaya na mkoa wa Kagera kufuatilia malalamiko ya wakulima ikiwemo kuwapatia vibali wakulima ambao wanasafirisha kahawa zao kutoka shamba moja kwenda jingine ili kuhakikisha haki inatendeka na kuondoa malalamiko yaliyopo hivi sasa juu ya vikosi kazi vilivyoundwa sehemu mbalimbali kufuatilia magendo ya kahawa.

Mwenyekiti wa Maandalizi ya Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Kagera, Respikius John alisema kuwa uwepo wa vyama vya ushirika mkoani Kagera umesaidia wakulima na watumishi katika vyama vya ushirika kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuepuka na mikopo umiza.

Alisema kuwa kwa Sasa Bei ya kahawa Safi yani Organic Arabika kilogram moja Sh 5,300 na Robusta ni 4,700 ukilinganisha na miaka 2 iliyopita kabla ya serikali kuamua kuuza kahawa ya mkulima kwa njia ya mnada ,kahawa ya maganda kilogram moja ilikuwa inanunuliwa kwa Sh 1,200 bila kujali kama ni kahawa safi ama hapana hivyo bei imepanda mara mbili zaidi na kuendelea kuongeza hamasa ya uzalishaji.

Alisema kuwa jukwaa la maendeleo ya ushirika lilofanyika Kagera ni la mara ya kwanza likiwa na lengo la kukutanisha wa vyama vya ushirika ili kueleza mafanikio na changamoto walizonazo ikiwa ni pamoja kupata mada mbalimbali kutoka Kwa wadau wa ushirika na viongozi wa serikali ambapo matarajio Ni kuhakikisha jukwaa Hilo linafanyika kila mwaka na kuchochoea zaidi hamasa ya kilimo cha kahawa chenye tija mkoani Kagera

Mrajisi msaidizi Mkoa wa Kagera Robert George alisema kuwa mpaka sasa mkoa huo una vyama vya ushirika 369 kati ya hivyo vyama vilivyo hai ni 288 na vyama ambavyo vinavyosuasua ni 81.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button