Walaghbishi Dodoma, halmashauri zatakiwa kukuza uchumi

DAR ES SALAAM :Mtandao wa jinsia nchini TGNP umewataka walaghbishi mkoani Dodoma kuhakikisha wanashirikiana na watendaji wa halmshauri katika mkoa huo kuwezesha programu za kuinua uchumi kwa vikundi vya wanawake ili kuhakikisha wanaleta usawa wa kijinsia katika mkoa huo.

Akizungumza wakati wa mafunzo kwa walaghbish kutoka mkoani humo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa jinsia nchini TGNP, Lilian Lihundi amesema endapo programu hiyo itatekelezwa kwa ushirikiano itakuwa msaada katika kuinua usawa wa kijnsia katika mkoa huo hasa ikzingatiwa mkoa huo upo chini kiusawa wa kijinsia .

Kwa upande wake meneja mradi wa tuinuke pa moja Nestory Mhando amesema mrado huo itatekelezwa hadi mwaka 2027 ambapo kwa sasa unatekelezwa katika halmashauri 3 za mkoa wa Dodoma ili kuinua kiuchumi wanawake ambao ndio waathirika wa tatizo la umaskini.

Nao baadhi ya walaghbishi kutoka mkoani dodoma Mwajuma Yahaya na Yusuph Athumani wamesema mafunzo hayo yatasaidia katika kujenga jamii kutambua masuala ya jinsia huku wakiwasihi wananchi kubadilika ili kukuza masuala ya usawa wa kijinsia .

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button