Walimu ndio msingi wa maendeleo – Biteko

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inautambua mchango wa walimu katika kujenga maendeleo ya Taifa.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko wakati wa sherehe ya siku ya Mwalimu duniani iliyoadhimishwa katika wilaya ya Bukombe na kuhudhuriwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda mkoani Geita.
Biteko amesema mchango wa walimu nchini ni mkubwa katika utoaji wa elimu na kwamba  walimu ni msingi katika kujenga uchumi.
Naye, Prof. Mkenda amesema katika kusheherekea Siku ya Mwalimu Duniani serikali itaandaa sherehe hizo ili zifanyike katika wilaya Bukombe Mwaka 2023.
Aidha, ameahidi kujenga Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA katika wilaya ya Bukombe ili kurahisisha kutoa msaada kwa wanachi wa Bukombe na Mkoa wa Geita.

Hafla hiyo imeandaliwa na Chama cha Walimu wilaya ya Bukombe nakuhudhuriwa na  viongozi mbalimbali wa Serikali ili kusheherekea kwa pamoja siku hiyo muhimu ya mwalimu duniani.

Habari Zifananazo

Back to top button