Walimu warahisishiwa ufundishaji Mtwara

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amekabidhi vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa na mradi wa BOOST ili kuwasaidia walimu katika kazi zao za ufundishaji kwa njia ya kisasa zaidi.

Tukio hilo limefanyika katika Shule ya Msingi Mitengo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani humo.

Amesema vifaa hivyo vitakuwa msaada mkubwa kwa walimu kujifunza mbinu mbalimbali za ufundishaji na ujifunzaji kupitia mpango endelevu wa mafunzo ya walimu kazini.

Amewataka walimu hao kuvitunza na kuvitumia vifaa hivyo kama ilivyokusudiwa.

Ofisa elimu mkoani humo, John Lupenza amesema vifaa hivyo vitatolewa kwa halmashauri zote tisa mkoani humo kwenye vituo vya mafunzo endelevu kwa walimu (TRC).

Vifaa vilivyokabidhiwa ikiwemo kompyuta 50, UPS 30 na printa 10 na kati hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba itapokea kompyuta 10, UPS 6 na printa 2.

Aidha halmashauri zingine zilizobaki zitapokea kompyuta 5, UPS 3 na printa 1.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Fidelis Kambanga amesema vifaa hivyo vitapunguza gharama mbalimbali ikiwemo kuchapisha mitahani ya wanafunzi.

Amesema kabla ya vifaa hivyo ikiwalazimu kutumia si chini ya Sh 300,000/- kwa kila mtihani mmoja kwa wanafunzi wote shuleni hapo.

“Kuprinti mtihani mmoja kwa kila mwananfunzi gharama yake ni shilingi mia 400/- ukizidisha kwa hiyo hela kwa kila mtihani mmoja gharama yake si chini ya Sh 300,000/- kwa shule moja”amesema Kambanga

“Ukizidisha kwa idadi ya shule ni kama Sh milioni 3.6 kwa mwaka mzima katika mitihani tunayoifanya”amesisitiza

Habari Zifananazo

Back to top button