Waliomba kujiunga na polisi wapewa maelekezo

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limewajulisha vijana waliotuma maombi ya kujiunga na jeshi hilo kutembelea mbao za matangazo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Kamanda wa Polisi Mkoa, Wakuu wa Polisi Wilaya na Wakuu wa Wilaya kwa ajili ya kuangalia majina ya walioitwa kwenye usaili.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi, Benjamini Kuzaga imeeleza usaili utaanza Agosti 21, 2023 saa 1:30 asubuhi katika ukumbi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mbeya.

Kamanda Kuzaga amesema kila kijana aliyeitwa kwenye usaili ahakikishe anaenda na vyeti halisi vya elimu, cheti cha kuzaliwa, cheti cha JKT/JKU, barua ya utambulisho kutoka kwa mkuu wa kambi kwa waliopo kambini, kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA, pamoja na pesa taslimu Sh 10,000 kwa ajili ya vipimo vya afya.

Habari Zifananazo

Back to top button