Zaidi ya wamarekani milioni 81 wajitokeza kupiga kura

MAREKANI : IDADI ya wapiga kura hadi sasa waliopiga kura nchini Marekani imefikia zaidi ya milioni 81 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Florida Election Lab.

Hadi kufikia leo siku ya kupiga kura, watu 81,379,684, tayari wameshapiga kura ambapo idadi ya wapiga kura milioni 44,402,375 wamepiga kura vituoni na milioni 36,977,311  wamepiga kwa njia ya posta.

Hatahivyo idadi ya wapiga kura imeonekana haitapita ile ya wakati wa janga la Covid ambapo ilizidi  kura zilizopigwa.

Katika mwaka 2016 kura zilizopigwa zilikuwa (milioni 47.2) na mwaka 2012 zilikuwa (milioni 46.2).

SOMA: Trump akana kubatilisha matokeo uchaguzi 2020

Habari Zifananazo

Back to top button