Wamiliki wa shule binafsi waonywa

MWANZA: WAMILIKI wa shule binafsi zenye mabasi ya kubebea wanafunzi wametakiwa kuboresha magari yao kwa kuyafanyia matengenezo ili wanafunzi wawe salama wakati wa kwenda shule na kurudi.

Aidha, wamepewa onyo kwa watakao bainika kuruhusu magari mabovu kuingia barabarani watachukuliwa hatua za kisheria.

Amri hiyo limetolewa leo Februari 24, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbroad Mutafungwa katika kikao alichofanya na wamiliki wote wa shule binafsi zilizopo mkoani humo.

Kamanda Mutafungwa amesema kuwa endapo atabaini gari bovu la kubebea wanafunzi linatembea barabarani atahakikisha halitaedelea na safari na badala yake wanafunzi hao watabebwa na magari ya polisi huku hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mmiliki wa gari hilo.

Aidha, Kamanda Mutafungwa amewaahidi wamiliki hao kuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani humo watafika katika shule zao kwa lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi walimu pamoja na madereva.

Mwenyekiti wa wamiliki wa shule binafsi wa mkoa huo, Laurent Samike amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendelea kudhibiti matukio ya uhalifu na kuhakikisha wananchi wanakuwa katika hali ya amani na usalama jambo ambalo limesaidia kupungua kwa vitendo vya kihalifu mkoani humo hasa mashuleni.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button