Wanachama TLP wapinga uongozi, msajili atoa siku 7

MSAJILI wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi ameupa siku saba uongozi wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kutoa ufafanuzi wa madai ya ukiukwaji wa katiba na kanuni za chama hicho.

Katibu Mwenezi wa TLP Taifa, Geofrey Stephen alisema hayo jijini Arusha jana wakati akizungumza na wanahabari. Stephen alisema wanachama wa chama hicho wamemwandikia barua Msajili wa Vyama vya Siasa wakip[1]inga uchaguzi uliofanyika Februari 2, mwaka huu Dar es Salaam.

Alisema wanachama hao wanadai uongozi wa taifa uliopo madarakani haupo kihalali. Stephen alisema wana[1]chama hao wanapinga uongozi huo kwa sababu viongozi wa taifa waliopo hawakuchaguliwa na wanachama halali na wanadai kuwa walichaguliwa na watu wa kuokoteza mitaani waliovalishwa sare za chama hicho.

Alisema TLP ina wanachama katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar na kwamba wajumbe 185 walistahili kupiga kura lakini waliopiga kura hawapo kwenye rejesta ya wanachama.

Stephen alisema taarifa ya kuhusu kufanyika Mkutano Mkuu ilitolewa siku mbili kabla ya mkutano huo kinyume na katiba na kanuni za uchaguzi za chama hicho na ilisababisha wajumbe wa mku[1]tano mkuu kutoka mikoa ya mbali washindwe kuhudhuria hivyo uchaguzi huo ni batili.

Alidai kuwa Mkutano Mkuu uliitishwa kwa ujanja ujanja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Richard Lyimo ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti bila kuwa na mpinzani licha ya nafasi hiyo kuwa na wagom[1]bea wengine.

Katibu wa TLP Mkoa wa Arusha, Kinanzaro Mwanga ambaye pia, alikuwa mgombea wa uenyekiti taifa alidai kuwa umefanyika uchaguzi wa ngazi ya taifa wakati ngazi za chini chaguzi hazijafanyika. Mwanga alisema kwa mujibu wa Katiba ya TLP toleo la 2009 uchaguzi unatakiwa kuanzia ngazi za chini na kumalizikia ngazi ya taifa.

Alidai kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa Katiba ya TLP hivyo uchaguzi huo ni batili na wanamuomba, Msajili wa Vyama vya Siasa aufute ili mchakato uanze upya kuanzia ngazi za chini.

Alisema kwenye barua yao kwa msajili imeeleza kuwa katika nafasi ya uenyekiti taifa kulikuwa na wagombea watano walio[1]pitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa Februari 5, mwaka jana kwenye kikao kilichofanyika makao makuu ya chama hicho Dar es Salaam.

Aliwataja wagombea hao kuwa ni Richard Lyimo, aliyekuwa Katibu Mkuu Taifa ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti na analalamikiwa kuvunja katiba. Wagombea wengine wa nafasi hiyo waliopitishwa ni Abu Chagawa, Ivan Maganza, Stanley Ruyamgabo na Kinanzaro Mwanga ambaye ni Katibu wa TLP Mkoa wa Arusha.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button