Wanafunzi 18,708 waliopata ujauzito wamerudi shuleni

DAR ES SALAAM: IKIWA leo ni siku ya mtoto wa kike Duniani , wanafunzi wa kike wa shule ya msingi na sekondari 18,708 waliopata ujauzito wamerudi kuendelea na masomo yao baada ya kujifungua katika kipindi cha miaka ya 2022 na 2023.

Mwaka 2022 wanafunzi 9,379 wa shule ya msingi walirejea shuleni baada ya kujifungua huku wanafunzi wa shule ya sekondari wakiwa ni 8154 na kufanya jumla yao kuwa wanafunzi 17,532.

Aidha mwaka 2023 wanafunzi wa kike 557 wa shule ya msingi walirejea huku wa shule ya sekondari wakiwa 619 na kufanya jumla ya walirudi shule kuwa 1176.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Doroth Gwajima amesema wanafunzi wanaorudi mashuleni baada ya kujifungua wasinyanyapaliwe badala yake wapewe ushirikiano.

“Nimekuja kusikiliza agenda zinazojadiliwa serikali inatoa elimu bure na waliokwama wanarejeshwa shule na sheria za elimu zinawezeshwa pamoja na uwezeshaji wa wanawake.

“Kuhusu sheria ya ndoa Dk Gwajima amesema waziri mwenye dhamana alisema wadau wametoa maoni kwaajili ya kuwasilishwa bungeni lakini kukawa na ushauri uliotolewa na kamati kwaajili ya kuboresha tutapata majibu mazuri kupitia bunge.”

“Changamoto zinazomkabili mtoto wa kike ni wanaishi katika ulimwengu wa digitali umekuja na changamoto nyingi watoto wa kike wanakutana nayo tutaongea zaidi kuhusu sheria ya kupambana na ukatili mitandaoni

Dk Gwajima amesema asilimia 67 ya watoto wenye 12 hadi 17 wanatumia mitando ya kijamii huku asilimia 4 ya watumiaji hao wamefanyiwa ukatili wa kimtandao.

“Suala lingine ni kudhibiti mitandao ya kijamii isiwapoteze watoto jamii ijiulize wazazi wameacha kulea wako kwenye shughuli za kiuchumi waangalie ni saa ngapi watalea na kutafuta uchumi wasiegemee upande mmoja.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Msichana Initiative, Rebeca Gyumi amesema miongoni mwa changamoto ni wazazi wengi wamekuwa hawatengi bajeti na kutoa huduma ili kukidhi mahitaji na wanaingia kwenye vishawishi na kupelekea mimba za utotoni.

Amesema watoto wa kike wanaingia kwenye ndoa za utotoni kwasababu sio chaguo la kwanza wanapendekeza serikali kuwekeza kwenye stadi za maisha na kujitambua kwa wasichana.

“Wamependekeza Kufanyia kazi sheria ambazo ni changamoto serikali kuwekeza watoto wa kike tangu wanazalowa kujua uwezo wao wanakuzwa kwa kujua uwezo wana na vitu wanavyofikia kama wasichana,”amesisitiza.

Habari Zifananazo

Back to top button