Wanafunzi Morogoro, Dodoma kupewa elimu stadi za maisha

WANAFUNZI wa shule za sekondari kutoka Halmashauri za Wilaya ya Malinyi na Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro pamoja na Chamwino, Dodoma wanatarajia kupatiwa elimu ya stadi za maisha kupitia mradi utakelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la Campaig For Female Educations (CAMFED).
Mradi huo unatarajia kutekelezwa mwaka wa masomo 2024 na unalenga kutatua changamoto mbalimbali za wanafunzi, kuthibiti mdondoko shuleni , kutojitambua na kuwaepusha kujiingiza kwenye vishawishi viovu.
Meneja Miradi wa Camfed, Latifa Sabuni amesema hayo mjini Morogoro wakati kikao kazi cha utoaji wa elimu kwa wakuu wa shule za sekondari 29 za Manispaa ya Morogoro na kuutambulisha mradi huo utakaotekelezwa katika halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Malinyi na Chamwino .
Shirika la Camfed limeazishwa mwaka 2005 na kusajiliwa mwaka 2006 na kwa sasa linafanya kazi kwenye mikoa 10 nchini katika wilaya 33.
Sabuni amesema, kwa sasa mradi wa ‘Life skills’ ni mpya kwenye shule hizo na haukuwahi kuwemo katika mradi unaofanyika na Shirika hilo .
Amesema wanafunzi hao watapewa stadi za maisha zitakazo wasaidia kujitambua na kujithamini kwa lengo la kupata elimu yao bila ya vikwanzo.
Sabuni amesema ni mradi wa kujitolea ambao utawatumia vijana waliohitimu shule ili kusaidia wenzao waweze kuendelea kubaki shuleni na kuchangia ufaulu uongezeka zaidi.
“Program hii itaanza Januari 2024, tupo kwenye maandalizi ya awali ya uchaguzi wa hao vijana , namna ya kuwafanyia mafunzo, lengo ni kuanza na wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaoanza mwaka wa masomo 2024” amesema Sabuni
Sabuni amesema mradi huo upo kwa ajili ya kulisaidia taifa letu katika kuwawezesha wanafunzi kujitambua watambue umuhimu wao wa kukaa shule , kuendelea na masomo na sio kuishia njiani kidato cha pili .
Naye mshauri wa Camfed na Mhadhiri Mwandamizi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Dk Siafu Sempeho amesema lengo ni kuhakikisha wanafunzi wenye dalili za kudondoka kutoka kwenye mfumo rasmi wa shule wanaweza kutambuliwa mapema na kusaidiwa ili kupunguza mdondoko.
Dk Sempeho amesema , watateuliwa wanafunzi waliomaliza shule na kupewa mafunzo ya namna bora ya kuwaongoza wenzao kwa kutambua viashiria vya mdondoko wa mapema .
Vijana hao watashirikiana na walimu wa unasihi shuleni na waongozaji wa wanafunzi ili mradi huo uweze kusaidia mzunguko wa elimu kuona wanafunzi wanaendelea kutoka darasa la saba hadi kidato cha kwanza , cha pili , nne na kidato cha tano bila kukwama njiani.
Dk Sempeho amesema ,kutakuwa na vikundi vya wazazi vitaundwa vikiwa na lengo la kuifanya jamii yenyewe ione inawajibika kusaidia watoto wao wabaki shuleni kwa kushirikiana na walimu na kufanya ubora wa elimu kuwa juu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa wakuu wa shule za sekondari Manispaa ya Morogoro, Festo Kayombo amesema wataandaa vipindi darasani na kuweka kwenye ratiba ya masomo la elimu stadi za maisha kwa wanafunzi ili kuwakinga na vihatasishi vinavyowazunguka wakiwemo bodaboda .
Working part-time and making an extra $15,000 or more online is a simple and quick method to gain money. I made $17,000 in the previous month by working in my spare time, and I am really satisfied now as a result of this job.
.
.
Detail Here——————————————————————–>>> http://Www.BizWork1.Com
HE/SHE DIED WITH CARDINAL RUGAMBWA HOSPITAL DISEASE… THE HISTORY OF THIS DISEASE WAS KILLED MORE THAN 5 MILION PEOPLE AROUND THE WORLD MANY WAS CHINESE, EROPEAN, KOREAN AND INDIANS… ALL WHERE WHITE SKIN PEOPLE
HE/SHE DIED WITH CARDINAL RUGAMBWA HOSPITAL “CONFERENCE” DISEASE… THE HISTORY OF THIS DISEASE WAS KILLED MORE THAN 5 MILION PEOPLE AROUND THE WORLD MANY WAS CHINESE, EROPEAN, KOREAN AND INDIANS… ALL WHERE WHITE SKIN PEOPLE…. KILICHOBAKI BABA/BWANA YESU ASIFIWE DISEASE
KWELI WEWE JAMAA KWAKO HAKUNA BAG
TUNZA MAZINGIRA YAKUTUZE… UTAKACHOONDOA NDIO KAZI..
100% KIWEKWACHO HUMO HUTENGENEZWA NA WANAWAKE
file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image002.jpg
file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image004.jpg