Wanafunzi wafundwa kujiajiri

WANAFUNZI nchini watakiwa kutumia elimu wanayopata vyuoni na vipawa walivyonavyo kujiajiri.

Hayo yamesemwa na Naibu Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Profesa Sotko Komba katika Kongamano la 11 lililofanyika Chuo cha Ustawi wa jamii jijini Dar es Salaam.

“Wanafunzi wanajengewa uwezo wa kutumia elimu wanayopata kugeuza kuwa fursa ya ajira kwao na kutoa ajira kwa wengi kwa kuthubutu na kuacha uwoga,”

Advertisement

“Kongamano limewahusisha Wanafunzi na wanazuoni ili kuwasaidia wanafunzi katika ubunifu na kutumia elimu waliopata kuwa fursa itakayo wasaidia katika kupata ajira na kujiajiri,”amesema Komba.

Pia ameongeza kuwa binadamu ni kiumbe anajifunza kila siku na kuzidi kupata uelewa na kubadilishana mawazo na kujua kutumia ubunifu na elimu walizopata.

Naye Helena Sailas Mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa jamii pia mwanzilishi wa uvumbuzi wa taka za plastiki kutumika kama maligafi katika ujenzi amesema kuwa Wanafunzi wanaweza kupata majibu ya maswali yao katika kuleta mabadiliko katika jamii.

“Nimefanikiwa kuvumbua kutatua changamoto ya plastiki kugeuza ajira na nimefanikiwa kutatua changamoto hiyo kwa kugeuza plastiki kuwa marigafi katika ujenzi na kutoa ajira kwa vijana wenzangu,”amesema Helena.

Kwa upande wake Mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi Junior Manguchie amesema kuwa mafunzo katika Kongamano hili yanatujrnga na yanasaidia Wanafunzi kusuluhisha matatizo yaliopo mtaani na jamii kuyapatia utatuzi.