MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Longido imetoa elimu kinga dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa wanafunzi 600 wa Shule ya Msingi Longido
Wengine ni wanafunzi 180 wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Samia iliyopo wilayani Longido katika Mkoa wa Arusha.
SOMA: Anaswa akijaribu kumhonga ofisa Takukuru
Wanafunzi hao walipewa elimu hiyo na ofisa elimu kutoka DCEA, Shabani Miraji juu ya madhara yanayotokana na matumizi ya dawa za kulevya na kuhimizwa kuepuka mazingira hatarishi na makundi ambayo sio sahihi ili kujikinga kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.
Pia, walihimizwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119.