Wanahabari wapatiwa mafunzo kuelekea Uchaguzi Mkuu

DODOMA : WANAHABARI wa Mkoa wa Dodoma wamepatiwa mafunzo ya usalama wa kimwili, kidijiti na afya ya akili kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Mafunzo hayo yametolewa kupitia Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC).

Mwezeshaji kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari Dodoma, Okully Julius, alisema waandishi wanapaswa kuwa makini zaidi kipindi cha uchaguzi kwa kuwa mara nyingi huambatana na vitisho na mashambulizi. SOMA: Inec yazidi kunoa wanahabari Uchaguzi Mkuu

Alisema ni vyema waandishi kuwajulisha watu wa karibu wanapokwenda kazini na kuchukua tahadhari dhidi ya mashambulizi ya kimtandao kwa kutumia nywila imara na uthibitishaji wa hatua mbili. Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha waandishi kutoa taarifa sahihi na kulinda usalama wao wakati wa kazi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button