Wanajeshi 84 DRC wapandishwa kizimbani

CONGO: KESI inayowakabili wanajeshi 84 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaotuhumiwa kwa mauaji, ubakaji, na uhalifu mwingine dhidi ya raia mashariki mwa nchi imeanza kusikilizwa.
Wanajeshi hao wanatuhumiwa kuvunja nyumba za raia katika vijiji vya Kabare na Kalehe, jimboni Kivu Kusini mwishoni mwa juma.
Timu ya mawakili wa wahanga, ikiongozwa na Pascal Mupenda, imesema wanajeshi hao wanadaiwa kuwabaka wanawake kadhaa na kuua takriban watu 12.
Hatahivyo, wanajeshi hao walifikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi huko Bukavu, jimbo la Kivu Kusini.
Kesi hiyo inasikika wakati waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wakizidi kushinda katika eneo la Kivu Kusini baada ya kuuteka mji wa Goma, jimbo la Kivu Kaskazini.
SOMA: Afrika Kusini yapeleka wanajeshi 800 Lubumbashi



