Wanajeshi walinda amani 15,000 kuondoka Congo

UJUMBE wa Umoja wa Mataifa wa kuleta amani nchini DR Congo (MONUSCO) umetia saini mkataba wa kuwaondoa wanajeshi 15,000 wa kulinda amani nchini humo.
–
Waziri wa Mambo ya Nje wa taifa hilo, Christophe Lutundula na Mkuu wa Monusco wametiliana saini makubaliano hayo Jumanne Novemba 21, 2023.
–
Katika mazungumzo yake na televisheni ya taifa, Lutundula amesema mpango huo unaashiria kufika mwisho wa ushiirikiano.
–
Wakati hayo yanajiri, wiki iliyopita Serikali ya Congo iliagiza jeshi la Kanda ya Afrika Mashariki kuondoka nchini humi ifikapo Disemba mwaka huu.



