Wananchi Nanyamba waombwa kuunga mkono juhudi za serikali

WANANCHI wa Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara wameombwa kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali hasa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yao.

Hayo yamejiri wakati wa mikutano ya hadhara iliyofanyika katika vijiji mbalimbali kwenye halmashauri hiyo iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota.

Miongoni mwa vijiji vilivyofanyika mikutano hiyo ni Misufini, Nachumu, Kiromba chini, Mikumbi, Kiromba na Mjimwema na vingine.

Lengo la mikutano hiyo ni kusikiliza kero mbalimbali za wananchi zinazowakabili katika maeneo yao pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya maji, elimu, barabara, umeme, elimu, afya na mingine

Akizungumza wakati wa mikutano hiyo ya hadhara, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya  Mtwara Vijijini, Nashir Mfaume amesema mikutano hiyo ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.

“Sisi serikali ya chama cha mapinduzi tunatekeleza miradi ya maendeleo kwa wigo mkubwa kutokana na zile ahadi ambazo tuliziahidi kwenu”amesema Nashir

“Niwaombe wananchi kuiunga mkono serikali yenu ya chama cha mapinduzi na miradi yote ya maendelelo inayotekelezwa kwenye maeneo yenu”

Hata hivyo wanapokuja viongozi na wataalamu kwenye kata zao wawaunge mkono kwasababu yale maendeleo wanayokuja kuwahimiza ni kwa faida zao wananchi hao.

Mbunge wa Jimbo hilo la Nanyamba, amesema wamekuwa na kasi kubwa ya utekelezaji wa Ilani hiyo kwani walikotoka siyo waliko sasa ambapo kuna mambo mengi  yamefanywa chini ya chama hicho.

Aidha amezungunzia moja ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye halmashauri ikiwemo wa umeme ambapo mpaka sasa vijiji vyote 87 jimboni humo vinawaka umeme pamoja na mitaa yote 9.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button