Wananchi Nanyamba watakiwa kufanya tathmini ya miradi
WANANCHI wa Halmashauri ya Mj wa Nanyamba mkoani Mtwara wametakiwa kufanya tathmini ya mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka 62 ya Uhuru hasa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyowekezwa katika maeneo yao.
Akizungumza leo mjini humo, Mbunge wa jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota amesema wamepitia Serikali za awamu mbalimbali ikiwemo sita ambayo ikijitahidi kuleta maendeleo kwa wananchi wake.
Hayo yamekuja wakati wa zoezi la kufanya usafi katika hospitali ya halmashauri ya mji huo na uchangiaji wa damu uliyofanyika Disemba 8, 2023 mjini humo.
Ameyataja mafanikio/ baadhi ya miradi ya maendeleo iiliyotekelezwa kwenye almashauri hiyo ndani ya kipindi hicho ikiwemo sekta ya elimu ambayo walikuwa na shule za msingi 7 na sasa zimefikia 69.
Shule za sekondari wakati wanapata Uhuru hawakuwa na hata moja ila sasa zimefikia takribani 13 na hivi karibuni wanarajia kufungua zingine 2 hivyo kufanya idadi ya 15 na shule moja ya kidato cha tano na sita.
Sekta ya afya awali hawakuwa na hospitali wala kituo kimoja cha afya ila sasa wana vituo vya afya 5 ikiwemo 4 vya Serikali na 1 binafsi, hospitali ya halmashauri 1.
“Ndio maana tunaona tofauti kubwa sana tulitoka na tulipofika sasa kwahiyo tufanye tathmini hali iliyokuwa kabla na ndani ya miaka 62 ya Uhuru kwa serikali za awamu zote ya kwanza mpaka sasa serikali ya awamu sita “amesema Chikota
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Walyama Tundosa amesema katika yaliyofanyika kwenye halmashauri kupitia sekta mbalimbali wamefikia zaidi ya asilimia 80 na bado wanaendeleza malengo yao kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mganga Mkuu wa halmashauri hiyo, Dickson Masale amesema hospitali inatoa huduma mbalimbali ikiwemo kwa akina mama wajawazito wanaokuja kujifungua na kwa siku wanakuja kati ya watano mpaka saba.